Raisi wa ufilipino ameagiza kufutiliwa mbali kandarasi wa kununua maelfu ya bunduki kutoka nchini marekani.Raisi huyo wa ufilipino bwana Butelte amesema taifa lake litatafuta njia mbadala ya kununua silaha hizo sehemu nyingine kwa bei nafuu.
Idara ya polisi ya ufilipino ilikuwa imepangiwa kununua bunguki takriban 26000 kutoka marekani.
Uhusiano baina ya nchi hizo mbili ambazo zilidumu kwa muda mrefu ila umedorola tangu raisi huyo aingie madarakani.
Kumekuwepo na taarifa kuwa marekani ilikuwa imepanga kutoiuzia ufilipino silaha izo kutokana na wasiwasi kuhusu ukatili wa raisi huyo wa ufilipino wa kukabiliana na walanguzi wa madawa ya kulevya.
Toka Raisi huyo aingie madarakani mtu yeyote akishikwa na madawa ya kulevya anapigwa risasi na kufa.
No comments:
Post a Comment