Tuesday, November 22, 2016

RAISI MTEULE TRUMP ASEMA MTOTO WAKE NA MKE WAKE HAWATAISHI WHITE HOUSE

Raisi mteule wa marekani wenyewe siku hizi wanamuita majina mengi mara Magufuri,wengine wanamuita Baba lao Wengine kubwa la maadui namajina mengi tu leo amevunja ukimya na kuzungumzia swala la mke wake na mwanae kutokuishi ikulu kwa sasa.

Na sababu yenyewe ya kwa nini mke wake pamoja na mtoto wao mwenyeumri wa miaka 10 kubakia katika jiji la New York,ni kwa ajili ya mwanao kumalizia masomo yake katika shule moja ya private iliyoko katika jiji laNew York.

Chanzo cha karibu kabisa na bwana Trump kililiambia gazeti la New York
post kwamba"Melania yuko karibu sana na mwanae Barron na wamekuwa na ukaribu sana hasa wakati wa uchaguzi"."Kampeni za uchaguzi wa Marekani imekuwa ngumu sana na imemuwia vigumu sana kwake kwa sababu ya mambo mengi yaliyokuwa yanaendelea mitandaoni hasa kuonekana kwa picha za utupu za mama ayake mtandaoni,kumemchanganya sana".Alisema
 Hata hivyo uamuzi wao wa kubaki katika nyumba ya bwana Trump utaongeza changamoto nyingi sana za kiulinzi,katika mamlaka ya ulinzi ya siri ya Marekani(secret service) na kitengo cha polisi(Police departiment),kwa sababu nyumba ya bwana Trump iko katika maeneo ya ubize mwingi sana.Na wanachama wa mtaa huo wanaweza kuingia katika jengo hilo na kutoka kama wanavyotaka.Ikumbukwe kwamba jengo hilo lilizungukwa na wapingaji wa matokeo pamoja na wanahabari wakiwemo polisi baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo.


No comments:

Post a Comment