Imefika wiki ya tatu sasa wananchi wa nchini korea ya kusini wakifanya maandamano wakiwa na hasira na kumtaka raisi wao aondoke madarakani.
Maandamano ya leo yanategemewa kuwa makubwa zaidi kutokana na taarifa iliyotolewa na viongozi wa maandamano hayo na kudai kuwa watu wengi sana watashiriki.
Maelfu wa polisi wanaodili na watu wanaofanya fujo wamepelekwa katikati ya jiji kwa ajili ya kupambana na waandamanaji hao
Raisi huyo anatuhumiwa kwa kuwa karibu na mfanyabiashara mkubwa choi soon anayetuhumiwa na mashtaka ya kutaka kuibia serikali kiasi kikubwa cha fedha kupitia kampuni kadhaa za taifa hilo.
Bi choi amekamatwa na kushtakiwa kwa kosa la ubadhilifu wa pesa za umma na matumizi mabaya ya mamlaka.
No comments:
Post a Comment