Mwanamama huyo amewashinda maraisi wa tatu wa Africa na kutangazwa hapo jana kuwa mshindi kwenye sherehe zilizoandaliwa nchini nairobi.
Bi Madonsela anasifika kwa msimamo wake mkali dhidi ya ufisadi alipokuwa anahudumu kama mlinzi wa maslahi ya umma Afrika Kusini. Alihudumu kuanzia mwaka 2009 hadi 14 Oktoba mwaka huu, muhula wa miaka sita
.
Kipindi hicho, alimchunguza rais, akawachunguza wakuu wa polisi, maafisa wakuu serikalini na hata wanasiasa wa upinzani.
Uchunguzi wake ulipelekea kusimamishwa kazi kwa mkuu wa polisi Bheki Cele mwaka 2011.
Aliwahi kumchunguza pia kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters Julius Malema ambaye mwishoni mwa kipindi chake, alimuunga mkono alipofanya uchunguzi kuhusu uhusiano wa Rais Jacob Zuma na familia tajiri ya Gupta.
Alimchunguza pia Rais Zuma kuhusu ukarabati uliofanyiwa makao yake Nkandla.
Bi Madonsela ni mama wa watoto wawili.
Alikuwa wakili na kiongozi wa vyama vya wafanyakazi wakati wa harakati za kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi.
Habari hii kwa hisani ya BBC SWAHILI.
No comments:
Post a Comment