Aliyekuwa nyota wa mpira wa kikapu wa marekani Dennis Rodman amejikuta akipata msala wa kugonga na kukimbia na kupelekwa maakamani kwa kosa hilo ambalo hukumu yake ni kifungo kisichozidi miaka miwili.
Nyota huy
o aliye na umri wa miaka 55 anatuhumiwa kwa kuendesha gari kwa kutumia arabara isiofaa huko kusini mwa jimbo la California ,swala lililolazimu gari jingine kukwepa na kugonga ukuta.
Waendesha mashtaka wanadaiwa kwamba Rodman baadaye alitoroka eneo hilo mnamo tarehe 20 mwezi Julai na kuwapa maafisa wa polisi habari za uongo.
Pia ameshtakiwa kwa kuendesha gari bila leseni.
Wakili wa Rodman,Paul Meyer anasema kuwa ajali hiyo ilitokea katika eneo
ambalo halina ishara za trafiki zinazoonekana.
Ameongezea kuwa Rodman alizuia ajali hiyo kwa kutogonganisha,kusimama na kuzungumza na watu waliokuwa ndani ya gari hilo.
Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea mnamo tarehe 20 mwezi Januari.
Rodman alishinda mataji mawili na klabu ya Detroit Pistons pamoja na ubingwa na timu maarufu ya Chicago Bulls katika miaka ya 90 akishirikiana na Michael Jordan.

No comments:
Post a Comment