Watazamaji wa anga wanategemea kuuona mwezi mkubwa duniani ambao walikuwa wanausubiri tangu mwaka 1948.
ingereza itakuwa na fursa nzuri kuuona mwezi huo siku ya Jumatatu
jioni,licha ya kuwa utakaribia dunia mwendo wa saa tano na dakika 21
muda wa GMT ambapo utakuwa umbali wa kilomita 356,509.
Wachunguzi
watauona mwezi huo kuwa mkubwa zaidi kwa asilimia 7 ukilinganishwa na
mwezi wa kawaida na kung'aa zaidi ya asilimia 15, licha ya kwamba macho
ya binaadamu yanaweza kupambanua tofauti hiyo.
Huku mwezi huo
ukitarajiwa kutokaribia dunia hadi tarehe 25 mwezi Novemva 2034, idara
ya maswala ya hewa nchini Uingereza imesema kuwa kutakuwa na mawingu
mazito wakati mwezi huo utakapokaribia.
Huku mwezi ukizunguka
dunia,kuna tofauti ya mwangaza unaotolewa na jua.Ni wakati huo ambapo
mwezi wote humulikwa na mwangaza huo na kutoa mwezi mkubwa zaidi.
BBC Swahili wameripot.
No comments:
Post a Comment