Thursday, November 24, 2016

STAA WA FILAMU WA INDIA AKUTWA ATM NA MTOTO WA NGURUWE

Nyota wa filamu kutoka nchini India ambaye kwa sasa yuko juu sana jana amesababisha mitandao nchini india kusambaa picha yake ikimuonesha akiwa katika kibanda cha kuchukua pesa maarufu kama ATM Akiwa amebeba mtoto wa nguruwe.

Ravi Babu amesema kuwa nguruwe huyo atashiriki katika filamu yake mpya kwa jin
a Adhigo ikimaanisha kutoka Telugo hadi ''there''.
Milolongo mirefu ya benki imekuwa kitu cha kawaida baada ya noti za rupee za 500 na 1000 kupigwa marufuku nchini humo katika vita dhidi ya ufisadi.
''Nilikuwa nikimpeleka ili kupigwa picha nilipogundua kwamba sina fedha za mafuta'',Babu aliambia BBC.
''Nilisimama katika eneo la ATM lakini nikalazimika kumbeba mimi mwenyewe baada ya kupiga kelele wakati msaidizi wangu alipojaribu kumbeba.Lazima umbebe ikiwa mkono wako uko katika kifua chake na umuweka karibu nawe ili ajihisi vyema''.
Picha hiyo imesambazwa katika mitandao ya kijamii nchini India.
kumekuwepo na visa vya ghasia nchini India tangu marufuku hiyo ya noti itangazwe ikiwa ni miongoni mwa harakati za kukabiliana na ufisadi wiki mbili zilizopita.
Watu wamekuwa wakipiga foleni kwa saa kadhaa nje ya benki pamoja na mashine za ATM ambazo huenda zikaishiwa na fedha.
Hatua hiyo imeathiri uchumi wa India.

No comments:

Post a Comment