Jamaa mmoja kutoka nchini marekani aliyejulikana kwa jina la Asher Woodworth kutoka katika jimbo la Maine nchini marekani amejikuta akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kuonekana na muonekano kama mti.
Polisi walimsindikiza pole pole mpaka kando ya barabara na kumuweka chini ya ulinzi.
Baada ya kukamatwa na polisi alijieleza na kuwaambia kuwa yeye ni muigizaji na nilipata wazo hili siku moja nilipokuwa natafakari na nikapata wazo hili na nikaamua kufanya hili jambo ili nishangaze tu watu na mavazi yangu haya.
Kijana huyo alitumia matawi mbalimbali akiwa pamoja na rafiki yake na walitumia masaa kadhaa kukamilisha vazi hilo namatawi hayo yalikuwa yananukia marashi mazuri.
Kijana huyo aliongeza kuwa yeye anapenda sana miti na alitiwa moyo sana na mpigapicha Charles Freger ambae alimpiga picha hii hapo chini Bbc swahili wameripot
Kijana huyo alikaa rumande masaa sita lakini baadae polisi walimwachia huru baada ya kugundua hana tatizo lolote ila alikuwa anajaribu kuonesha tu vazi hilo.
No comments:
Post a Comment