Mkali kutoka jijini Mabatini Jijini mwanza HAMISI BABA aka H.Baba leo kupitia kipindi cha xxl kwenye kipengele cha UHEARD Amesikika akimponda mkali kutoka Madale bwana Diamond aka Simba.
Kupitia ukurasa wa instagram jana bwana diamond alipost video akiwa kwenye nyumba yake hiyo ambayo amenunua nchini south africa na nimara ya kwanza tangu anunue nyumba hiyo ndo alikuwa amefika hapo,baada ya muda zilizagaa picha zingine ambazo zilimuonesha king kiba akiwa amekaa kwenye nyumba ambayo ilisemekana kuwa niyake.
Sasa H.baba ilibidi apost na kuandika kuwa anachojua yeye mtu akinunua kitu basi inatakiwa apost na hati ya kitu alichonunua ikiwemo na ushaidi wa manunuzi hayo.Akiongea sa soud brown wa xxl Mkali huyo kutoka mwanza alidai kuwa Diamond anatakiwa aonyeshe hati kama kweli amenunua nyumba hiyo sio kumuona mwenzake kapost nayeye anaamua kupost anatakiwa apost na Hati ya nyumba hiyo kama kweli anania ya kujulisha uma kuwa amenunua mjengo huo sio bra bra tu.
Kwa upande wa alikiba baada ya kupigiwa simu kwanza alishangaa na akadai yeye hana nyumba yeyote na kwanza anaishi kwenye nyumba ya kupanga.
Mkali huyo wa AJE aliongeza kuwa hata kama ananyumba hawezi ku show off Ni show off ili iweje nimuoneshe nani?ALI KIBA ALIMALIZA.
No comments:
Post a Comment