Tuesday, October 25, 2016
MAAJABU HAYA YAMTOTO ALITEZALIWA MARA MBILI
Mtoto mchanga nchini marekani amezaliwa mara mbili baada ya madaktari kumtoa katika mfuko wa uzazi wa mama yake kwa dakika ishirini na kumfanyia upasuaji,Katika miezi minne ya mimba ya mtoto huyo mama yake aligundua kuwa mwanae anauvimbe kwenye uti wa mgongo.
Uvimbe huo ambao unajulikana TERATOMA Ulikuwa unasukuma damu kutoka kwa mtoto huyo jambo ambalo liliongeza hatari ya moyo wa mtoto huyo kutofanya kazi.Pindi anatolewa tumboni mtoto huyo alikuwa na uzito wa chini ya kilo moja.
Mama huyo awali alibeba mimba ya mapacha lakini alimpoteza mtoto mmoja kabla ya miezi mitatu ya kwanza na awali madaktari walimshauri aitoe mimba hiyo kabla hawajamfanyia upasuaji huo wa hatari.
Lakini madaktari hao wamefanikisha upasuaji huo na mtoto amezaliwa tena upya akiwa salama na ameruhusiwa na yuko nyumbani anaendelea vizuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment