Serikali ya nchini gambia imedai nayenyewe inafata msimamo wa Burundi kwa kujitoa kwenye mahakama ya uhalifu ya kimataifa ya ICC.Madai hayo yamekuja baada ya nchi za africa kulaani kuwa mahakama hiyo inashugulika na nchi za Africa pekee.
Nchi hiyo imetamka tamshi hilo baada ya hapo juzi kuona South Africa nawao kujitangaza kujitoa kwenye mahakama hiyo.Raisi wa Gambia amekuwa madarakani toka mwaka 1994.
Uchaguzi mkuu wa nchi hiyo inategemewa kufanyika mwezi wa kumi na mbili mwaka huu viongozi wa upinzani wanne wamekamatwa na kuukumiwa miaka mi 3 jela kwa kosa la kufanya maandamano yasiyo na kibali.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu limesema kuwa maamuzi hayo ni sehemu ya mchakato wa kuendelea kukandamiza haki za binadamu katika taifa la Gambia.
No comments:
Post a Comment