Monday, October 24, 2016

KENYA YASHAMBULIWA TENA

Mji wa mandera unaopatikana mpakani mwa Somaria na kenya umevamiwa na wanamgambo na kushambuliwa na kusababisha mauaji ya watu kadhaa.Polisi wanadai milipuka mitano ilitokea kabla ya ushambuliaji wa risasi kutokea.Eneo hilo lililoshambuliwa huishi watu ambao wengi wao sio jamii ya wasomari.

Maafisa wapolisi wamedai mpaka sasa niwatu wanne wamekufa na watano kujeruhiwa na mji huo umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa alshabab.

Polisi na wanajeshi kwasasa wanafanya msako mjini humo BBC Swahili wameripoti.

No comments:

Post a Comment