Monday, October 24, 2016

JUSTIN BIEBER AZIRA KUPAFOM NA KUSHUKA JUKWAANI KWA HASIRA.

Mkari kutoka US Justin Bieber alijikuta anashuka jukwaani kwa hasira katika shoo yake mjini Manchester baada ya mashabiki wake kumkera na kelele ambazo walikuwa wanazipiga ambazo yeye hakufuraishwa nazo.

Mkali huyo alisema kuwa nathamini mchango wenu mnaonipa nathamini ukarim wenu lakini kelele mnazopiga wakati mimi naimba naomba mzisitishe sidhani kama nivema naposema kitu nyinyi mnapiga kelele.Lakini mashabiki hao hawakumuelewa kabisa ndipo mkali huyo alipoamua kutupa kipaza chini na kushuka jukwaani huku mashabiki hao wakiendelea kumzomea.

Lakini baadae kijana huyo machachari alirudi jukwaani na kuwaeleza mashabiki wake kwanini alishuka jukwaani na akaendelea nashoo yake ambayo watu walikuwa wengi sana.


No comments:

Post a Comment