Saturday, October 29, 2016

SUGE KNIGHT BADO ANAMTAKA DR DRE AMLIPE ASILIMIA 30 YA MAPATO YAKE.


Producer mkongwe Duniani DR DRE amejikuta akiingia matatizoni baada ya Producer mwenzake mkongwe Suge kumpeleka mahakamani kwa kile kitendo ambacho anadhani dr dre ndio aliyepanga shambulizi ambalo alinusulika kufa.

Suge anadai alikuwa na mkataba wa kusimamia kazi za dr dre na alitakiwa alipwe asilimia zake kwenye mapato ya beats by dre.Suge anadai dre alimlipa jamaa pesa na akatekeleza na suge alipigwa risasi mara saba tumboni lakini suge hakufa.

Polisi walimuhoji mtu ambaye alijulikana kama T money na aliwaeleza wapelelezi kuwa alilipwa na dre pesa ili amuue suge,na suge analalamika kuwa kwenye club hiyo kulikuwa na camera 37 lakini hakuna aliyeshikwa.

Suge amefungua kesi na anamtaka dr dre amlipe asilimia 30 kwenye mauzo ya beats by dre ambayo nisawa na dola milioni 300,na dr dre anamiliki dola bilioni moja.

No comments:

Post a Comment