Saturday, October 29, 2016

MILLARD AYO APEWA TUZO NA TAASISI YA GHF

Mtangazaji wa clods fm na Mmiliki wa AYO MEDIA Bwana millard ayo leo hii amekabidhiwa Tuzo na taasisi ya GREAT HOPE FOUNDATION Kwa kuwa mfano wa kuigwa.

Tuzo hizo zilizopewa jina la onesha uwezo zimetolewa leo na Mgeni mwalikwa JONH OLANGA amesema kuwa mtangazaji huyo amekuwa nimfano wa kuigwa kwa vijana sababu alipambana sana mpaka kufikia mafanikio aliyoyapata leo.

Ameongeza kuwa millard alishawai kufanya kazi bila kulipwa kwa muda mrefu na kukatishwa tamaa na wazazi wake lakini alipambana na leo hii amekuwa mfano wa kuigwa maana amefikia hatua ya kumiliki Media yake na ameajiri vijana zaidi ya kumi.

MKATAVI.BLOGSPOT.COM Tunakupongeza kwa tuzo hiyo na endelea kupambana ili uweze kutupa nasisi changamoto katika tasnia hii,Mungu akubariki sana.+

No comments:

Post a Comment