Tuesday, August 15, 2017
ONA MAAJABU YA SAMAKI WA DHAHABU WANAOTENGENEZA POMBE
Wanasayansi wamefanya utafiti wao nakugundua samaki wa ajabu ambao wanaishi chini ya maziwa ambayo yamefunikwa na barafu juu.
Wanasayansi hao wamegundua pia uwezo wahali yajuu wa samaki hao kugeuza Asidi ya lastik kwenye miili yao na kufanya kuwa pombe ambayo pombe hiyo huitumia kuwafanya waendelee kuishi.
Kwa mujibu wa BBC Swahili wameripoti kuwa Samaki hao waligunduliwa na kiwango kikubwa cha pombe ambacho kinazidi hata kile cha Dereva anachostairi kuwa nacho mwilini kwenye damu katika nchi nyingi.
Watafiti hao wameongeza kuwa kutokana na samaki itawasaidia kuendelea kufanya utafiti zaidi kujua madhara yanayotokana na pombe kwa binadamu.
Pia watafiti hao wamedai kuwa samaki hao wa dhahabu wanauwezo wa kuishi kwenye mazingira magum kama kukosa oxgen wenyewe wanauwezo wakuvumilia hali hiyo kwamiezi kadhaa lakini binadamu hata saa moja hawezi kufikisha bila oxgen
Samaki hao wanapatikana baharini kaskazini mwa bara la ulaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment