Monday, August 28, 2017

KICHWA ALEX OXLAIDE KUJIUNGA NA CHELSEA?

Kiungo kutoka ARSENAR Mwenye umri wa Miaka 25 kwasasa Alex Oxlaide anategemea kujiunga na kikosi cha Chelsea.

Chelsea imekataa kutoa tamko lolote kuhusu mshambuliaji huyo lakini inasemekana mambo yote yameshakamilika.


Liverpool pia walikuwa wakimtaka mchezaji huyo na bado wanaweza kuwasilisha ombi la kuvutia ili kumnyakua mchezaji huyo.
Oxlaide Chamberlain amecheza kila mechi ya Arsenal kufikia sasa msimu huu ikiwemo kichapo cha 4-0 ilichopata Arsenal dhidi ya Liverpool wakati alipotolewa.
Kiungo huyo wa kati atakuwa mchezaji wa 5 wa Chelsea kusajiliwa kufuatia kuwasili kwa Alvaro Morata, kipa Willy Caballero, beki Antonio Rudiger na kiungo wa kati Tiemou Bakayoko.

No comments:

Post a Comment