Katika mitandao ya kijamii toka majuzi zilikua zinasambaa habari ambazo sizo rasmi kuwa kutokana na matengenezo yani marekebisho ambayo yanafanywa uwanja wa taifa kuwa limepatikana fuvu la mtu.
Lakini Alex Mkenyenge mkurugenzi msaidizi wa idara ya michezo amepinga uvumi huo nakudai kuwa lile sio fuvu.
Kwanza hiyo ni taarifa ya uongo na
hakuna fuvu isipokuwa ni madude ambayo yamepatikana kwenye mchanga baada
ya kuwa tumefukua sehemu ya uwanja, kwa hiyo hakuna kitu kinachoitwa
fuvu la mtu wala nini ni madude tu yaani mamimea yale yaliyooza basi
yanafanana kama magimbi ambapo ndani lilikuwa limeshaliwa”
“Sasa kwa sababu mtu analiona kwa mbali anasema fuvu sasa
sijui fuvu litakujaje hapa, kwanza kilichotokea hilo dude limekuja na
mchanga wala halikuwa ndani ya uwanja, yaani kwenye mchanga uliyoletwa
ambao tulikuwa tunajaza kwenye pitch baada ya kuwa tumeondoa lea ya juu”
Kwa hiyo hakuna kitu kama hicho bahati
mbaya kwa watanzania wanapenda kuzungumza vitu vibaya kuliko vizuri,
maana mtu haulizi wala kushangaa ile inayosafisha uwanja, sasa kama ni
fuvu unataka kusema uwanja wa Taifa kulikuwa na makaburi?”
Nb.Chanzo cha habari na millardayo.com.
No comments:
Post a Comment