Waziri mkuu Casim Majariwa Casim ameomba apewe maelezo yakutosha kuusu faru maarufu kwa jina la Jonh ambaye hajulikani alipo huku tetesi zinasema faru huyo ameamishwa nawengine wanadai amekufa.
Bw Majaliwa amewataka viongozi wa NCAA kuwasilisha kwake nyaraka zote
zilizotumika katika kumuhamisha faru huyo kufikia Alhamisi.
Alisema ana taarifa kuwa faru huyo John alihamishwa kwa siri na kupelekwa Grumeti katika eneo Serengeti mnamo 17 Desemba, 2015.
"…
mliahidiwa kupewa shilingi milioni 200 ambapo mkapewa shilingimilioni
100 kwa ahadi ya kumaliziwa shilingi milioni 100 nyingine baadaye,"
alisema Bw Majaliwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily News la
Tanzania, Bw Majaliwa alisema kwa miezi mitatu sasa, hakuna taarifa
zozote kumhusu faru huyo ambazo zimetolewa.
"Naomba niletewe
nyaraka zote zilizotumika kumuomba na kumuondoa faru huyo na barua
zilizotumika kujadili suala la faru John. Nasikia amekufa naomba pembe
ziletwe ofisini na iwapo itathibitika aliondoka bila ya kufuata taratibu
wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria,".
Bw Majaliwa
pia alimsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa NCAA, Sezzary Simfukwe kutokana
na tuhuma za ubadhilifu wa fedha zinazomkabili.
Kwa sasa, anahojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
"Haiwezekani
mtumishi awe anachunguzwa na Takukuru halafu aendelee kuwa ofisini si
atavuruga uchunguzi. Asimamishwe kazi kuanzia leo mpaka hapo uchunguzi
utakapokamilika na aikibainika kwamba hana hatia atarudi kazini,"
alisema.
Hifadhi ya Ngorongoro ndilo eneo pekee Tanzania ambapo faru wanapatikana kwa wingi porini, ndani ya kreta.
Inakadiriwa kwamba idadi ya faru katika hifadhi hiyo ni takriban 35.
HABARI HII NI KWA HISANI YA BBC SWAHILI.
No comments:
Post a Comment