Mkali kutoka nchini Ningeria bwanamdogo machachari anayejulikana kwa jina la WIZ KID Amejikuta akikabiriana na kesi ya kutokutokea kwenye shoo nchini Uganda.
Wizkid alishindwa kutokea kwenye show iliyokuwa ifanyike December 3 mwaka huu mjini Kampala. Kampuni iliyomlipa, Face TV, kupitia mwanasheria wake, Fred Muwema,
imepata kibali cha kumkamata muimbaji huyo kwa kuchukua dola $60,000 na
kushindwa kutokea kwenye show. Gharama zingine walizotoa ni brokerage
fee, $5,000 na per die, $3,000 kwa muda ambao Wizkid angekaa Uganda.
Muimbaji huyo alidaiwa kushindwa kusafiri na ndege toka Marekani kwenda nchini humo kwa show hiyo.
Zaidi ya watu 25,000 walikuwa wamenunua tiketi kwaajili ya show hiyo. Maelezo yaliyowasilishwa mahakamani yameeleza kuwa mwandaaji wa shiw hiyo amekula hasara ya zaidi ya $300,000 kutokana na maandalizi aliyofanya.
No comments:
Post a Comment